News
Loading...

Hatimaye Swetu Fundikira atalala pema peponi


Marehemu Swetu Fundikira
Baada ya kuahirishwa toka tarehe 30/102012 mpaka tarehe 20/11/2012 hukumu ya kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira leo asubuhi ilifikia tamati kwa Mh  jaji Zainabu Mruke kuwapata na hatia ya kumuua kwa makusudi Swetu Fundikira.
Jaji Mruke akisoma ushahidi wa pande ya mashtaka na ile ya utetezi alisema"Hakuna shaka kwamba hakuna mtu aliyeshuhudia(aliyeona) Swetu Fundikira akiuawa, hivyo katika hali kama hii ushahidi wa kimazingira ndio utakao pelekea kuthibitisha jambo hili pamoja na utetezi wa washitakiwa .
Lakini je, maelezo ya washtakiwa yanajitosheleza kuondoa shaka juu yao kuwa hawakuhusika na tukio hili? Katika hali ya kawaida hapa pana shaka kwa maelezo ya mshtakiwa wa pili Ali Ngumbe kwamba mtuhumiwa wa kwanza Rhoda alilewa hivyo hakuweza kuendesha gari hivyo ilibidi yeye(Ally) aendeshe kasha Rhoda arudi na gali hilo kutokea maeneo ya Ukonga airport hadi maeneo ya drive in ni dhahili kuwa jambo hili lilikua haliwezekani

“SHERIA:Melezo yasiyokidhi haja na yenye utata kwa upande wa ushahidi ni faida kwa upande wa mashtaka(Jamhuri)” Jaji alinukuu sheria
Pia kwa hali ya kawaida pamoja na kwamba hakuna aliyeona Swetu akiuawa lakini majeraha aliyokuwa nayo kichwani (marehemu) yanawafanya na kusababisha (washtakiwa) watoe maelezo na ushahidi wa kina bila kuacha shaka, jambo ambalo katika ushahidi wao limeonekana kutia shaka ya hali ya juu kuwa wao wamehusika na hali hiyo.
Ushahidi wa washitakiwa haukuweza kukata mnyororo wa mtiririko wa ushahidi hivyo kufanya mkono wa hatia kuwaelekea wao kuwa ndio walio sababisha kifo cha Swetu.
Ukirejea mtiririko wa ushahidi uliotolewa na mashahidi wote watano ambao umeweka mtiririko wa mnyororo ambao haukukatishwa na utetezi unatosha kuwa uthibitisho wa mauaji katika mahakama hii
MAZINGIRA YA KESI:
• Ushahidi umetengeneza mnyororo
• Ushahidi umeshindwa kutoa matundu
NIA OVU:
Katika kesi hii ya mauaji NIA OVU imethibiti katika mambo yafuatayo:
• Rhoda(mshitakiwa) alipotoa kauli ya kumwambia Sopstenes walipokuwa Mango kuwa “Usipoheshimu wakuu wan chi utaumia”
• Rhoda(mshitakiwa) alipotoa kauli ya kuwaambia wenzake kuwa “wale washenzi hawa hapa niliwaambia mwatie adabu mnaona sasa wametufuata mpaka huku?”
• Swetu kushambuliwa na watu watatu
• Watuhumiwa kujitambulisha kuwa wao ni wanausalama lakini hawakutenda jambo lolote la usalama
• Majeraha ya kichwani aliyokutwa nayo Swetu(a very sensitive area)
• Kumdhalilisha Swetu kwa kumuacha uchi wa mnyama
• Maneno ya washitakiwa kabla na baada ya tukio yalikua ni ya kijeuri na kikorofi wala hawakujutia kilichotokea.
Kwa maelezo haya haiwezekani kusema kuwa wamefanya jambo hili bila ya kukusudia(wameua kwa kukusudia)
Mheshimiwa Jaji aliomba kwa heshma na taadhima kutofautiana na wazee wote wa mahakama ambao wote kwa nmyakati tofauti wamekua wakitoa kauli za kuonyesha washtakiwa hawakukusudia na wamebambikiwa kesi kwa kusema kuwa wote watatu(washitakiwa) wamefanya/wamemuua Swetu Ramadhani Fundikira kwa kukusudia.
KOSA: Kosa limethibitika kwa ushahidi ambao hauna shaka hata kidogo kuwa washitakiwa wote watatu kwa pamoja wanahatia ya kumuu Swetu kwa kudhamiria:

WAKILI WA UTETEZI:
Kutokana na mazingira ya kesi hii naomba mahakama iwapunguzie adhabu wateja wangu kwa sababu kwamba wote ni vijana na wanahitajika katika ujenzi wa Taifa hili, wanategemewa na familia zao pia mazingira yenyewe ya kesi
Baada ya washitakiwa kuambiwa wamehukumiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia walipewa nafasi ya ya kusema neno lolote nao walisema mmoja mmoja kwa kuomba wapunguziwe adhabu.
Baada ya Jaji(Mh. Zainab Mruke) kuwasikiliza alitoa ufafanuzi kuwa pamoja na maelezo yote watuhumiwa wanapaswa kujua kua kuna nafsi imetolewa duniani kwa dhuluma (A SOUL HAVE BEEN LOST) na kama imethibitika mauaji ni ya kukusudia hukumu huwa ni moja tu kuuwawa ,akawaomba watu wate waliohudhuria mahakama kusimama na akatamka adhabu yao kuwa ni 
KUNYONGWA HADI KUFA 
TUNASHUKURU HAKI IMETENDEKA TENA KWA MUDA AMINA!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :