News
Loading...

Mnyonge namnyonga


Tumeona mara nyingi mnyonge hunyongwa na haki yake huporwa na wajanja wachache, lakini hapa kwa kijana wa Keronyingi, Mnyonge hunyongwa na haki yake hupewa. Picha hizi mbili hapo chini zinaonyesha ujenzi wa awali wa barabara itakayounganisha vitongoji viwili vya Msisiri A na kwa Kopa vilivyopo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar. Kwa miongo mitatu niliyoishi mnaeneo haya eneo hili lilikuwa kama kijibwawa ambapo palipitika kwa wenda kwa mguu tu, lakini kuna watu huko halmashauri wameona umuhimu wa sehemu sasa kuendelezwa na kuwa barabara itakayopunguza misongamano katika barabara kubwa zipitazo maeno haya hasa nyakati za asubuhi na jioni. Hongereni sana kwa hili lakini msianze kuwa kama Mgema, akisifiwa tembo hulijaza maji. Hapana, napenda niwafahamishe kuwa jicho langu lipo hapo kufuatilia maendeleo ya ujenzi huu hadi pale itapofunguliwa rasmi. Kipande kifupi tu hiki jamani hata kilometa moja hakina, mwaka mpya iwe tayari basi.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :