News
Loading...

Msanii wa wiki!


Wapendwa wadau blogu lenu pendwa limeanzisha kipande cha msanii wa wiki ambapo kila wiki tutamuhoji msanii mmoja wa Bongo flava na kisha tutayaweka mahojiano hayo humu, tunatumai mdau utanufaika na majibu atakayoyatoa msanii husika. Na kwa kuanzia leo hii tunaanza na msanii Amini Mwinyimkuu.


 
Amini Mwinyimkuu Aka Nduli.
 

Mambo Amin?
Poa!
Mkala hapa kutoka keronyingi blog.
Aah kaka inakuaje?
Mzuka mwingi tu, sasa Amin nina maswali machache ya kukuuliza na majibu yako natumai yatawanufaisha wadau wa blogu hili na mashabiki wako kwa ujumla.
Haina noma kaka we uliza tu.
Ok, naanza kama hivi :
1. Una uhusiano wa  aina gani na Linah?
No comment!
2.Kuna uhusiano gani kati ya wimbo wako wa Nikimbie na wa Linah Bora nikimbie?
Uhusiano upo tena mkubwa, mimi ndiye niliyetunga nyimbo hizo mbili! 
3.Kwa hiyo unasemaje kuhusu uvumi kuwa una matatizo na Lina ndio maana mkaimbiana hizo nyimbo?
Kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa mimi ndiye nilitunga nyimbo hizo na nikampa moja Linah aimbe na hatuna matatizo yeyote.
4.Lini unataraji kutoa single mpya na inaitwaje?
Mwezi Januari 2011 nitatoa single mpya iitwayo Yameteka dunia anbayo nimemshirikisha Mwana Fa! Pia mwezi huo huo wa kwanza nitaitambulisha albam yangu iitwayo Yameteka dunia yenye nyimbo 10 pale mlimani City.
Amin nashukuru sana na nakutakia mafanikio mema katika kazi zako za muziki katika mwaka mpya wa 2011!
Nashukuru sana kaka!


 

Amin na Linah.

 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :