News
Loading...

Off side Bowyer!
 

<><><> 
<><><> 
HOT STREAK ... Dimitar Berbatov fires his eighth goal in three games
Dimitar Berbatov akifunga goli lake la 14 na la
kuongoza dhidi ya Birmingham City
ambao hata hivyo walisawazisha kupitia
Lee Bowyer kwa bao lenye utata.
Lee Bowyer mchezaji kiungo wa Birmingham city na mchezaji wa zamani wa mahasimu wa Man United, Leeds United alifunga bao la kusawazisha katika dakika za lala salama dhidi ya Man united na kuufanya mchezo huo kuisha kwa suluhu ya bao moja kwa moja katika uwanja wa Mtakatifu Andrew jijini Birmingham. Pamoja na picha za marudio kumuonesha  
Lee Bowyer akiwa ameotea yeye pamoja na wenziwe wanne huku Nikola Zigic akiunawa mpira huo kabla kumpasia Bowyer ambaye aliukwamisha mpira huo wavuni na kumuwezesha Allex Mc Leish kumnyima pointi tatu kocha wake wa zamani katika timu ya Aberdeen ya Scotland Sir Allex Ferguson ambazo zingemuwezesha kujichimbia mbali zaidi na wapinzani wake wa karibu katika kugombea ubingwa wa Barclays Premier League. Hata hivyo Man united walikaribia kujipatia goli la pili kupitia Berbatov lakini kiki yake kali iligonga mwamba na kutoka nje. Na kwa matokeo hayo Man united bado inaongoza ligi hiyo inayosadikika kuwa kuwa bora zaidi ulimwenguni kutokana na kuwa vilabu vya nchini humo hasa Man united na Arsenal kuwa na  wapezi wengi duniani kuliko timu zingine katika mabara yote saba hapa ulimwenguni. Kilabu cha Man united kinakadiriwa kuwa na mashabiki wasiopungua 30 milioni na pia ndicho kilabu chenye thamani kubwa zaidi kwa kukadiriwa kuwa na  thamani ya pauni za kiingereza bilioni moja na nukta tano.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :