News
Loading...

Je Tabora ina wapenzi wengi wa Taarab kiasi hiki?


Tangazo la onesho la Hadija Kopa

Tangazo la onesho la Jahazi ya Mzee Yusuf
Je kupeleka Tabora maonesho mawili ya muziki wa taarabu katika usiku mmoja ni sahihi? Katika hali ya kawaida maonesho huweza kugongana kwa kuwa waandaji wapo wengi katika mji wetu wa Tabora lakini hata ikitokea basi busara ishike hatamu, wawili hao wakae wajadili jinsi ya kutatua tataizo hilo. Lakini katika hili naona kama kuna kiburi au tamaa kimejengeka ama kwa waandaaji wote wawili au mmoja, nasema hivi kwa kuwa najua tangazo gani kati ya hayo mawili juu pichani ndilo lilikuwa la kwanza kuonekana kwa zaidi ya mwezi ndipo jingine likaja ibukia pasipojulikana. Kwa hiyo ni dhahiri kuwa muandaaji mmoja anatumia umaarufu wa Bendi moja ya taarabu kumtia hasara mwenzie. Nafahamu fika kuwa hakuna sheria iliyovunjwa na muandaaji yeyote hakatazwi kufanya onesho siku yeyote lakini kuna suala la ubinadamu pia ni la kuzingatiwa. Maoni yangu nafikiri umefika muda sasa waandaji wa maonesho Tabora wawe na kalenda ambapo kila mtu atajua lini mwenzie analeta onesho gani ili haya maombo yasijirudie.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :