News
Loading...

Asha Baraka akata miti apanda miti, Julio alonga.Rapa machachari Juakali
akimwaga vionjo vyake.

Venance akionyesha umahiri
wa kuiga sauti ya Chokoraa.

Haji Ramadhani akisalimia
washabiki wa Twanga Pepeta.
Mpiga besi gitaa Gody Kanuti
alipotambulishwa kujiunga na
 Twanga Pepeta.
Baada ya Mkurugenzi wa The African Stars Band (Twanga Pepeta) Bi Asha Baraka kuwafukuza kazi rapa Khalid Chokoraa na mwimbaji Kalala Junior takriban wiki nne zilizopita kwa kilichoelezwa utovu wa nidhamu, hatimaye ameajiri vipaji vipya vinne waimbaji wawili na marapa wawili.Kwanza alitambulishwa Haji Ramadhani kutoka Bongo star search ya mwaka juzi ambaye anaonyesha kipaji kikubwa hasa akitulia na kuzingatia miiko ya uanamuziki.wa pili kutambulishwa akawa Venance ambaye alionyesha umahiri mkubwa kuiga sauti ya Khalid Chokoraa na wa tatu akawa rapa na dansa mkali Juakali aliyetokea TOT Plus ambaye ana vipaji kadhaa kama alivyowaonesha mashabiki wailofurika katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar siku ya jumamosi ya tarehe 15/1/2010. Katika hatua nyingine ya kunogesha utambulisho huo wa wanamziki wapya Mwalimu wa soka mwenye maneno mengi Jamuhuri Kiwelu(Julio) alipanda jukwaani na kuueleza uma uliojazana hapo kuwa Chokoraa na Kalala wamekosea tu na watarudi Twanga eti kwa kuwa Bendi za mjini hapa Tanzania ni Msondo Jazz Band na Twanga Pepeta tu hivyo walipoenda sipo.


Wadau wa Twanga ambao majina
 yao hayakuweza kupatikana.

Mcheza sinema Jacob Stephen
na Said Mdoe Screen Masters.
 

Asha Baraka na Jamuhuri Kiwelo
mdau wa Twanga pepeta.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :