Baada ya muda usiozidi
mwaka mmoja tangu Swetu Fundikira auawe tarehe Ijumaa 22/1/2010 na askari jeshi watatu Sajini Rhoda Robert, Mohamed Ngumbe na Ally Ngumbe ambao ni ndugu kesi hiyo sasa inatarajiwa kuanza kuskilizwa hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo katika Mahakama ya Kisutu Bi Monica Mbogo kesho siku ya jumanne ndipo itahamishwa rasmi kwenda mahakama kuu kwa kusikilizwa an hatimaye kutolewa hukumu. Swetu Fundikira alikutwa na mkasa huo na hatimae umauti akitokea Kinyaiyas Pub iliyopo Kinondoni vijana nyuma ya Mango Garden. Kifo chake kimeleta simanzi kubwa kwa familia yake, jamaa na marafiki.Pia aliwahi kushindwa kitatanishi katika chaguzi mbili kuu za mwaka 2000 na 2005 akigombea nafasi ya udiwani wa kata ya Mwananyamala. Katika kuonyesha umahiri wa mtu huyu baadhi ya wana familia wa ukoo wa kitemi wa Fundikira wamekuwa wakisema kifo chake kimewanyag'anya Chifu wao wa baadae. Kwa waliomfahamu vema Swetu alipenda watu,michezo, muziki na siasa na hasa haki na kutetea wanyonge. Na wanakubali kuwa Taifa limepoteza kiongozi mahiri ambaye alipendwa na wengi na wengi walipendelea kumwita Mheshimiwa, pamoja na kuwa hakuwahi kupata kuwa mheshimiwa katika siasa. Umahiri huo ndio uliwafanya viongozi wa ngazi mbali mbali wa CCM akiwemo baba yake mkubwa Hayati Alhaj Chief Abdallah Fundikira kumshawishi ajiunge na chama hicho kikongwe, lakini yeye aliamini asingeweza kutetea wanyonge kama angejiunga na CCM na ndio sababu aligoma kukihama chama cha Wananchi CUF ambapo mpaka anakufa alikuwa mwanachama hai wa chama hicho. Katika mazishi yake palihudhuriwa na watu wapatao 2000 hivi umati ambao tumezoea kuuona wanapokufa viongozi wa nchi. Swetu ameacha watoto watatu wote wa kike Misuka 26, Syalo 24 na Sivuno Swetu Fundikira mwenye miezi minane. Sivuno hakuwahi kumuona baba yake kwani alizaliwa baada ya Bw Swetu Fundikira kuwa marehemu miezi kadhaa iliyopita. Swetu Fundikira atatimiza mwaka mmoja tangu afariki siku ya tarehe 24/1/2011 katika hospitali ya Muhimbili (ICU) ya idara ya mifupa MOI alifariki kufutia majeraha ya ndani ya kichwa ambapo alikuwa na internal bleeding. Mungu aiweke pema peponi roho yake kaka yetu kiongozi wetu na mtetezi wa wanyonge hayati Mh Swetu Ramadhani Fundikira. Amin!
0 comments :
Post a Comment