Sijaelewa busara gani ilitumika kupeleka kiwanda cha sigara Dar ikiwa zao hilo linapatikana Tabora hasa ukizingatia kuwa mkoa huo una kiwanda kimoja tu cha nyuzi, na ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa mkoani humo, kiwanda cha sigara kingeleta tofauti kubwa sana kwa wakazi wa mji huo mkongwe na uliosahauliwa ama kwa kusudi au utashi wa kisiasa wa watu fulani katika serikali ya awamu ya kwanza. Tuna karibu miaka 50 tangu tupate uhuru ambao mkoa huo ulichangia mno upatikanaji wake lakini ndio kwanza mchakato umeanza kuzitia lami barabara ziingiazo mjini Tabora. Mimi naona hii ni aibu kubwa kwa serikali zote zilizopita na iliyopo. Lakini huenda si aibu kwao, kama walipanga kuiadhibu Tabora kwa utashi wao wa kisiasa wataonaje aibu? Tabora ndipo ipo shule ya sekondari waliposoma viongozi wengi wa nchi hii wakiwamo J.K. Nyerere, Alhaj Chief A.S. Fundikira na Ibrahim Lipumba nikitaja wachache tu.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
5 comments :
Mkala hilo nalo neno maana apo akuna uzalendo Mwanawane.Yani kama wame isusa TB
Mdau wako A.Maganga
Almasi ichimbwe Mwadui, kiwanda cha kukatia kipo Iringa Tancut; pamba ilimwe Shinyanga, kiwanda cha nyuzi kipo Iringa, COTEX; wakulima wapo nyanda za juu kusini, kiwanda cha zana za kilimo kipo Ubungo Dar-es-Salaam(ok, kuna branch yao Mbeya ilijengwa baadaye). Zote hizi ni katika sera za wakati ule ambao pia uliwatoa wanafunzi wa Songea waende shule ya sekondari Moshi, na yule wa Musoma aende shule ya sekondari kiufundi Mtwara; yule wa Bukoba aende Kibaha sekondari. Zote sera tuu.
Nadhani kitu bora ni kutafuta jinsi ya kuwekeza kwenye tumbaku hapo hapo tabora , asali na mazao yote yanayopatuikana tabora ndio wengine wataona hasaraya kupeleka mazao sehemu nyingine!Mimi nampango huo, nitaanza na kimoja baada ya kingine...
Nashukuru kwa comments wadau, keep it up!
usikate tamaa, endelea kuipamba tabora!
Post a Comment