Hapa ni kwa dada Mage Urban quater, Uzunguni jana pakiwa hapana watu kama juzi na siku zingine za nyuma ambapo watu walifikia mpaka 4500 katika foleni. Sijui hali hii inamaaanisha nini lakini nitaendelea kufuatilia maendeleo ya mahudhurio ya wahitaji kikombe mahala hapa. Hata hivyo barabarani nilikuta basi dogo likiwa limejaa watu wenye asili ya ki Asia wakanambia wametoka kunywa dawa kwa dada, walionesha kuwa na furaha sana hatimaye kujipatia kikombe. Mmoja wao kwa jina Sudhesh alisema walitokea Mwanza. Ila walikataa kupigwa picha nami nikaheshimu ombi lao hilo!
Hili basi dogo lilisheheni watu wenye asili ya kiasia.
Watu wamegundua da' Mage feki nini? Mbona big drop ya watu, au wote wameshakunywa. Naomba utusaidie ushuhuda wa watu waliopata kikombe cha "babu" da' Mage.
3 comments :
Kaka asante sana kwa picha, umenikumbusha mbali sana, hata shule ya Msingi niliyosoma, asante sana.
Mdau
Canada
Never mind bro,
just anytime!
Watu wamegundua da' Mage feki nini? Mbona big drop ya watu, au wote wameshakunywa. Naomba utusaidie ushuhuda wa watu waliopata kikombe cha "babu" da' Mage.
Post a Comment