News
Loading...

Jaydee yupo katika daraja la peke yake!


 
Jukwaa jipya la Machozi Band.

Jaydee na Seven katika
uzinduzi wa maji yake.


Maji ya kunywa yenye jina la Jaydee.

Mwanadada Judith Wambura Habash aka Jaydee amedhihirisha kuwa mwaka uliopita ulikuwa wake kimafanikio katika jukwaa la mziki na nje ya jukwaa hilo, Judith ambae ameolewa na  mpenzi wake wa muda mrefu aliyekuwa mtangazaji wa Clouds fm 88.4 Bw Gadna Habash. Jaydee ambaye pamoja na bendi yake kufanya vema kisoko na uwingi wa mashabiki katika show zake tatu katika wiki ambazo ni Savanah Lounge Alhamisi, Mzalendo Pub ( kiwanja cha nyumbani) Ijumaa na Sweet Easy Jumapili. Kwa show hizi tatu tu, Jaydee anaweza kuwa anaingiza si chini ya Tsh milioni tano kwa kila wiki iendayo kwa Mungu. Ni pengo kubwa sana kati yake na wasanii wenzie wa Bongo Flava waliobaki. Na kama yote hayo hayatoshi katika kujikita mbali na wenzie amenunua jukwaa jipya na la kisasa kwa ajili ya Machozi Band ikiwa pale Mzalendo Pub siku za ijumaa pia anatarajia kufungua mgahawa wa kisasa maeneo ya Ada Estate utakaoitwa Nyumbani Lounge. Na katika kupigilia msumari mafanikio yake sasa amezindua maji ya kunywa yenye jina lake yatakayouzwa pale Mzalendo Pub. Na kwa vyovyote Gadna anahusika sana na maendeleo haya hasa kwa kuwa yeye ndiye meneja wa Jaydee. Na wiki chache zilizopita tumeshuhudia Gadna akiacha kazi pale Clouds fm ambako amekuwa kwa karibu miaka kumi hivi, nafikiri yote hayo ni kutokana na majukumu ya kibishara kumzidi na ndipo alipoona ni busara kuacha kazi hiyo ya utangazaji iliyomshuhudia akipanda na na kushuka vyeo mara kadhaa.
Kwangu mimi Jaydee ndiye msanii mwenye mafanikio kuliko wote kwa miaka kadhaa sasa lakini muhimu zaidi ni mwaka uliopita 2010. Na natarajia kuona Mwanadada huyu akitanua wigo wa biashara zake ifikapo mwishoni mwa mwaka huu mpya wa 2011 huku akifanya vema katika sanaa ya muziki.
Big Up Jide! 


Jaydee akionyesha kitega
uchumi chake kipya maji
 yenye jina lake.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :