Katika hali ya kustaajabisha kuna Mzee fulani maeneo ya Ukonga jijini kwa miaka mitano sasa amekuwa akitaka kuuza kiwanja chake kikubwa kwa bei rahisi lakini ameshindwa kupata mteja kwa muda wote huu hivyo akaniomba nimtangazie humu. yafuatayo ni masharti ya mnunuzi kufuata mara atakaponunua kiwanja hicho chenye ekari mbili na kinachouzwa kwa shilingi halali za ki Tanzania zipatazo miliont 3.5 tu.
1. Ikitokea umefanya sherehe yeyote nyumbani kwako pombe marufuku!
2. Upikapo chakula hakikisha unakipima ipasavyo ili kuepuka kutupa katika pipa au shimo la taka.
3. Na ukijaaliwa kujenga ghorofa hata moja, utalazimika kuwaezekea kwa mabati majirani zako wote kuepuka wewe na watoto wako kuwachungulia majirani wanapoenda ama kujisaidia au kuoga.
Ukiweza kuyatimiza masharti haya kiwanja ni chako!
0 comments :
Post a Comment