News
Loading...

Facebook ni hatari kwa watumiaji!



Mark Zuckerberg mmiliki
wa Facebook bilionea mwenye
 umri wa mika 26 tu.
 
 
Facebook mtandao maarufu
 zaidi wa kijamii duniani.
 Mtandao wa Facebook unaomilikiwa na Mark Zuckerberg ambaye hadi kufikia mwaka 2010 alikuwa na rasilimali zenye kufikia dola za kimarekani bilioni 6.9 na hivyo kumfanya kuwa bilionea mwenye muri mdogo zaidi. Kiasili ni Mmarekani mwenye asili ya Kiyahudi. Mwaka 2004 yeye na wenzie wanne aliosoma nao katika chuo kikuu Havard waliuanzisha mtandao huo kwa pamoja na Zuckerberg akiwa CEO wa Facebook. Mtandao huo umeelezwa kuwa hatari kwa watumiaji hasa wale waishio nchi zilizoendelea hasa katika mabara ya Ulaya, Australia, masharki ya mbali na Marekani ya kaskazini. Hatari hizo ni pamoja na kwa mfano pale mtumiaji anapojieleza mtandaoni humo kuwa anasafiri kwenda katika fukwe za Hispania kwa wiki mbili, kwa mtu mwenye nia mbaya na wewe atalifurahia jambo hilo kwani tayari atakuwa anajua hukai na mtu na anaweza akaingia nyumbani mwako kwa nafasi, pengine akakuibia na kufanya mengi yasiyofaa katika nyumba yako ukiwa safarini. Na kumbuka Katika mtandao huo kuna watu wa aina tatu nao ni watakaokutafuta kwa sababu za kibiashara, pili ni ndugu na marafiki zako na tatu ni maadui zako ambao hutokana miongoni mwa marafiki zako. Mtu hawezi kuwa adui yako kama hamjuani hata chembe.  Pia imeelezwa unajiweka katika hali ya kuibiwa tarehe zako za kuzaliwa ambapo katika mabara niliyoyataja hapo juu mabenki ili kukupatia huduma fulani huuliza maswali yanayofanana na yanayoulizwa na Facebook unapojiunga nao. Hilo huwawezesha maadui zako kupata taarifa nyingi kuhusu wewe, unaweza ukajiuliza ni vipi wapate details zako? wakati wewe umezitoa kwa Facebook tu? Kuna watu wana uwezo wa kuzipenya system ngumu ikiwa ni pamoja na za mabenki na ndio sababu wizi wa kimtandao unashamiri pande zote za duniani. Cha msingi ni kuwa mwangalifu na yale uyafumbuayo katika mtandao huo maarufu duniani ili adui zako ambao mara zote hutokea miongoni mwa watu wako wa karibu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :