News
Loading...

Asha Baraka amjibu Choki!


Mkurugenzi wa ASET BI Asha Baraka.


Leo hii katika ofisi za bendi ya ASET kampuni inayomiliki bendi ya African Stars Twanga pepeta Asha Baraka mbele ya vombo lukuki vya habari alizungumzia mambo kadhaa juu ya bendi hiyo ni pamoja na kumjibu mmiliki wa bendi ya Extra Bongo kuwa Twanga pepeta si bendi ya msimu kama ilivyo Extra Bongo ambayo kuanzishwa na kufa ni kitu cha kawaida kwa kwao.
“Twanga ni mti wenye maembe matamu hivyo kwa kitendo cha Ally Choki kuchukua wasanii wa bendi hii sishangai kwani alianza chochoko hizo muda mrefu na wapo baadhi ya wasanii waliolipwa fedha muda mrefu hivyo tulijua kuwa wataondoka”.
Asha anaendelea kwa kusema kuwa hana kinyongo na wasanii walioondoka bali anawaombea dua njema na kutaka watumie vyema fedha walizopewa kwa sababu ni za msimu siyo endelevu.
Twanga hatutaki malumbano, sanaa ni vipaji hivyo hapa ASET wapo wasanii wengi ambao ni wasomi lakini wameamua kubobea katika sanaa na ukikata mti tunapanda mti wale wameondoka wengine wanaendeleza gurudumu.Wakati huohuo amesema kwamba bendi hiyo haiendeshwi kwa majina au kwa jina la msanii fulani kwa sababu wasanii wake wote ni nyota na wana uwezo sawa hakuna makundi kama wengi wanavyoweka matabaka kwa wasanii.
“Hapa Twanga kila mtu analipwa mshahara hakopwi mtu au kumshusha huyu ukampandisha msanii mwingine” anasema.
Akizungumzia kuhusu bendi ya Extra Bongo kuchukua wasanii wake alisema kuwa ana hakika na anachokisema kuwa hiyo ni bendi ya msimu kwani anajua kwamba ipo siku itavunjika kama ilivyovunjika ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza.
“Nasema hivi Choki hatonikomesha mimi , mimi ni mwanasiasa, mfanyabiashara nina fedha kumshinda yeye na hata huyo mama ambaye analetafujo hivi sasa katika biashara ya muziki, muziki siyo chuki kama wanavyofanya wao labda waje wanichome kisu hapo kweli lakini vinginevyo hawaniwezi” alisema Asha Baraka kwa kujiamini.
“Wanahabari hebu angalieni historia za bendi zoote hapa nchini Twanga haijawahi kufa lakini Extra Bongo iliwahi kufa na sasa wameibuka huku wakitegemea kunyakua wasanii wa Twanga ili walikamate soko,ni jambo lisilowezekana Twanga ina historia yake” alisema Asha.
Wakati huohuo alimpongeza Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT),Ruge Mutahaba kutokana na jinsi alivyoweza kuwaibua wasanii na kulikamata soko, pia amempongeza na Mkurugenzi wa Benchmark Productions Rita Poulsen kutokana shindano lake la Bongo Star Seach (BSS), vijana wenye vipaji wapo kwa nini watu hawataki kuwavumbua walikotoka na kuchukua wasanii wa wenzao?
Aidha amemsifu msanii mdogo kuliko wote katika bendi hiyo Martin Kibosho kutokana na uamuzi wake wa kutoihama bendi hiyo alisema, namsifu Kibosho kwani mara alipoitwa na kupewa fedha kiasi cha sh. mil 6 alizigawa katika bahasha na kulinganisha pato lake la mwaka na kugundua kwamba hazitaweza kukidhi matakwa yake ya kila siku licha ya kwamba amekuwa akipokea vitisho kila kukicha jambo lililopelekea kuzima simu yake ya kiganjani.
Mwisho Asha amemtangaza Kassim Mohammed (Super K) , kuwa kiongozi wa wanenguaji wa kiume ambapo amerithi mikoba ya Supa Nyamwela na Lilian Tungaraza ‘Internet’ kuwa kiongozi wa wanenguaji wa kike.
Hamis Kayumbu ‘Amigolas’ ambaye Meneja wa matukio na uhusiano, kiongozi wa bendi ni Luiza Mbutu akisaidiwa na Saleh Kupaza ambaye pia ni mhakiki tungo wa bendi hiyo ambayo imeshangaza wengi kwa umaarufu wake kuongezeka pale ilipopoteza wasanii wake nyota kama Kalala junior na Khalid Chokoraa walioanzisha bendi yao na rapa Rogert Hega (Katapila) na Paul John (Fagason) aliyetimkia Extra Bongo pamoja na madansa kadhaa.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :