Kutoka kushoto Haji Ramadhan,Luiza Mbutu,Venance na Kimobitel
Aliyekuwa kiongozi wa bendi ya Extra Bongo Hadija Mnoga aka Kimobitel ameihama bendi hiyo na kujiunga rasmi na Twanga pepeta leo hii asubuhi. Akilielezea jopo la vyombo vya habari lililofika hapo alisema kilichomuondoa Extra Bongo ni pamoja na kukosa mshahara kwa muda mrefu na kutwishwa zigo la kuwafukuza kazi wanamuziki wa zamani saba wa bendi hiyo ili kupisha wale nane kutoka Twanga ambao yeye anaamini wamesaidia kwa kiasi kikubwa kuiweka bendi hiyo hapo ilipo. Pia alieleza kutoridhishwa na hatua ya Ally Choki kuwalipa pesa nyingi wanamuziki wapya na kutowapa chochote wao akiwemo yeye ambao wamekuwa na bendi hiyo kwa hali na mali lakini jitihada zao hazikutambuliwa na mmiliki wa bendi hiyo. Pia palikuwepo na Gody Kanutiakitambulishwa tena kurejea Twanga baada ya wazazi wake kumkataza asihame Twanga na hivyo kusababisha arudishe milioni sita za bendi hiyo.
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Ash Baraka akisisitiza kitu.
Mpiga solo mahiri Gody Kanuti.
Aliyekuwa kiongozi wa bendi ya Extra Bongo Hadija Mnoga.
Habari na picha ni kwa hisani yabongoweekend.blogspot.com
0 comments :
Post a Comment