News
Loading...

Mapacha watatu coco!Bendi chipukizi inayoundwa na wanamuziki wabunifu na wenye talanta za hali ya juu vijana Jose Mara, Khalid Chokoraa na Kalala Junior jana jumanne ilifanya show Coco beach kama ilivyo ada ambapo kila siku ya jumanne hufanya onesho kata ukumbi huo. Kwa kifupi tu na kwa taarifa yenu wapinzani wa bendi hiyo kwa vipaji vilivyopo katika bendi hii nathubutu kusema wataitaifikisha mbali bendi hiyo kama Mapacha wataweza kuhimili mikiki mikiki ya siasa chafu za muziki wa dansi nchini hapa kwani wapo wanaofikiria kubomoa bendi fulani tu na si kujenga bendi tokea chini. Na hao ni kama Manchester City, Chelsea na Real Madrid wa muziki wa dansi, mfano ni timu hizi hutaka ready made tu na sio kuwachukua vijana wakiwa wadogo na wenye vipaji na kuviendeleza mpaka wafikie kupevuka. na niionavyo mimi bendi hiyo baada ya mwaka mmoja hivi itafanya vema sana katika soko, pamoja na kuwa bendi hiyo hutegemea wapenzi wa bendi zingine za dansi hapa mjini Dar ndio waje kuingia katika maonesho yao. Na hili linaeleweka! Endeleeni kujituma mfikie mafanikio mafanikio ili mtimize ndoto zenu!  
Big up Mapacha!

Josee Mara , Kalala Junior na wanenguaji wa bendi hiyo.

Mpiga gitaa wa Mapacha!

Songoro Fundikira mimi na Josee Mara.
Rapa Khalid Chokoraa na wanenguaji wa Mapacha.

Baba na mwana

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :