Jana katika uwanja wa taifa Taifa stars iliikaribisha timu ya taifa ya Palestine katika mchezo wa kirafiki ambapo Stars ilishinda kwa golo moja bila kwa goli lililofungwa kifundi na Mrisho Ngassa baada ya kupasiana vema na Mohamed Bamka Simba. Goli hilo liliufanya uwanja huo mkubwa na wa kisasa katika pande hizi za dunia ulipuke kwa kelele hasa kutokana na goli lile lilivyokuwa zuri kama yale ambayo tumekuwa tukiyaona katika English Premiership.
0 comments :
Post a Comment