News
Loading...

Fagason badala ya kuacha msiba, aacha harusi Twanga pepeta!


Asha Baraka akijadili jambo na
wanamziki Shakashia na Saleh Kupaza
Katika hali iliyoshangaza wengi nikiwemo mimi jana ndani ukumbi wa Mango garden, ilikuwa shamra shamra kama bendi hiyo imepata mwanamziki mpya, lakini ukweli ni kuwa bendi hiyo imepoteza mwanamziki rapa Paul John (Fagason) masaa kama 72 yaliyopita kabla ya onesho hilo la jana jumamosi zilitapakaa habari kuwa Fagason, Rogate Hega, Gody Kanuti, wanenguaji Super nyamwela na mwanadada Otilia bendi ya Ally Choki Extra Bongo. Hatimaye zilithibitika kuwa kweli. walikuwa wametwaliwa na bendi hiyo.
Majira kama ya saa nane na nusu usiku hivi Luiza Mbutu akatangaza kuna kitu anataka kuwaonesha wapenzi wa Twanga waliokuwa wamefurika na ulipofikia muda akamwita Gody Kanuti jukwaani ambaye alikiri kupewa sh milioni sita (6,000,000) ili aihame Bendi hiyo na ajiunge na Extra Bongo lakini alisisitiza kuwa hataki kuhama Twanga na akazitoa pesa hizo pale jukwaani ambapo baadaye alikabidhiwa Asha Baraka. Pia Kanuti ambaye ndiye alipiga gitaa la solo katika wimbo Mwana Dar es Salaam alipewa gitaana na akachombeza kidogo jambo ambalo liliwakuna sana mashabiki wa bendi hiyo ukumbini humo. Kana kwamba hiyo haikutosha Diof naye kaja na Rapu mpya ya Kamata mwizi, ukweli ni kuwa Msafiri Diof kila inaposemekana kwmba kaisha kimuziki yeye huibuka na kitu kipya kama alivothitisha tena jana. Rapu yake hiyo ilipokelewa vizuri na mashabiki kwani kwa uchache Diof labda aliondoka na kama laki mbili hivi za kutunzwa tu. Katika hatua nyingine alipanda jukwaani Kocha wa dunia na kupagawisha mashabiki kiasi kwamba wakaanza kupiga mayowe kwa Luiza Mbutu kwamba achukuliwe Twanga Pepeta. Alimradi tuliokuwemo mle Mango Garden jana tulipata raha za kutosha. Luiza Mbutu aliahidi kulipeleka ombi la washabiki kwa uongozi likajadiliwe na katika hali isiyokuwa ya kawaida jana mziki ulizimwa saa saa 9.45 za usiku badala ya saa iliyozoeleka saa 9 kamili.

Amigolas na Janet Isinika.

Jamani Twanga rahaaaaaa!

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa ASET Omari Baraka na Noel


Mdau wa Twanga Chosta
  na rafiki yake.

Mimi na Q-Chila ndani
ya Twanga city.

Wapenzi na mashabiki wa Twanga pepeta jana.

Kiongozi wa bendi ya African stars
 Luiza Mbutu akionesha umma
sh milioni sita alizopewa na xtra bongo
mpiga solo wao Gody Kanuti.


Pesa za Extra Bongo hizi hapa.

Wadau wa Twanga wakishuhudia
Gody Kanuti akizirudisha sh 
milioni sita za Xtra bongo kwa
Kiongozi wa Twanga Luiza Mbutu.

Kamata mwizi. ni staili mpya ya rapu ya Msafiri Diof

Asha Sharapova.
Kocha wa dunia kati kati.

Wanenguaji mahiri.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

MAMBO YA MUZIKI BWANA !!YAANI DIOF ALIDHARAULIWA SANA TWANGA HADI AKAANZA KUSAHAULIKA,SASA SHIDA IMETOKEA TWANGA KUKIMBIWA NA IDADI KUBWA YA WANAMUZIKI,DIOF AMEKUWA "MTU"AJABU !!!!

Anonymous said...

Huo ni upuuzi,sasa kuna maana gani ya kuonyesha kitita cha pesa hadharani,mambo mengine huwa hayana hata maana,tena huyo Kanuti ni mjinga wa mwisho atakuja kujutia ujinga aliofanya,anaona sifa kurudisha pesa,wenzio wanakimbia bendi wewe ndio unavimba kichwa kwenda kujitumbukiza kwenye mtego,bull shittt !!!!!!ni ujinga mtupu.
Mwananyamala ,dar