News
Loading...

Kitu gani kitamfanya kiongozi serikalini ajiuzulu?


Edward Lowassa.

Nazir Karamagi.

Ibrahim Msabaha.
Tangu waziri mkuu aliyejuzulu kwa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond Mh Edward Lowassa na vijana wake wa kazi Bw Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha sijaona tena mtu mzito akijiuzulu pamoja na kuwa kumetokea madudu ya hali ya juu nchini humu na yametokea tena jana katika kipindi hiki lakini mabwana wa chama kikongwe wanapenda madaraka kama walizaliwa nayo.Tumeona milipuko ya mabomu ya jana lakini wahusika wameng'ang'ana kimya kana kwamba kilichotokea si kibaya cha kuweza kuwawajibisha. Hii si bahati mbaya bali ni uzembe kazini, hawa mabwana walijua kilichotokea mwaka juzi 2009 Mbagala lakini hawakuhamisha mabomu hayo ya mwaka 47 ambapo inaekea ni ya kizamani mno kiasi kwamba ukiingia ghalani mnamohifadhiwa mabomu hayo ukipiga chafya tu yanalipuka. Wahusika walikuwa na muda wote duniani wa kuhakikisha mabomu yote yanahamishiwa mbali na makazi ya raia lakini wangejali vipi kama wao hawaishi maeneo hayo? Na hali itaendelea mpaka wananchi watafikia kuwalazimisha wahusika wajiuzulu wanapoharibu. Lakini kwa sasa tugange yajayo. Eh Mungu wape nafuu wale waliojeruhiwa na mabomu ya kizamani na warehemu wale waliopoteza maisha kwa uzembe wa watu wachache! Pia nakuomba ewe Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma umpe Rais wetu uwezo na ujasiri wa kuwafukuza kazi wale wote waliozembea kuhamisha mabomu yetu ya kizamani.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Mohamed Kiswagara said...

I can't agree with you more , but this is not about Mwinyi and Mwamunyange , this is about Kikwete , these are his people , he should have fired them right away .People have been killed , properties been destroyed , businesses been disrupted . I suspect if you go deep and investigate you might find out there is some kind of ufisadi been involved. But I would push for those victim be compensated everything they lost and for those who lost their life , their relative should be compensated too.