News
Loading...

Mkono wa Rais Kikwete ni mzito sana!


Wapendwa wadau kuna mmoja wenu ame comment katika makala niliyoi post humu yenye kichwa Ni kitu gani kitamfanya kiongozi ajiuzulu serikalini? Yeye kama mimi ana fikiri ilikuwa ni busara kwa Waziri wa ulinzi Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Bw Davis Mwamunyange wafukuzwe kazi mara moja kwa kuwa ndio hasa watu wakuu waliopewa dhamana ya jeshi hilo na maafa haya yametokea kwa mara nyingine tena katika muda usiozidi miaka mitatu hivi. Hii ni dhahiri mabwana hawa hawakufanya kazi vile wanavyopaswa kufanya. Mh Rais Kikwete alitakiwa awape saa 48 kama hawajajiuzulu kwa ridhaa zao binafsi basi awafukuze kazi kwa kuwa yeye ndiye aliyewapa nyadhifa hizo kama dhamana na sio kama zawadi au ni zake yeye binafsi ambapo anaweza kumpa amtakaye au anaweza akamuacha katika wadhifa huo hata kama anaharibu kama walivofanya Dk Mwinyi na Davis Mwamunyange. Mchangiaji wa makala hayo pia anongeza kwa kusema anatarajia kuona wahanga wote wanafidiwa na serikali kuanzia wenye ndugu waliopoteza maisha, mali zilizoharibiwa na biashara zilizosimama kutokana na maafa hayo. Nafikiri mimi naunga mkono kwa aslimia 100 anachokisema kuwa serikali iwafidie wahanga wote kwa kuwalipa fedha taslim na hii itakuwa fundisho kwa serikali na ambayo labda mara nyingine itakuwa makini juu ya masuala mbali mbali kama haya ambayo imekuwa si makini katika kuyashuhulikia.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :