News
Loading...

Mpoki azua kizaazaa katika uteuzi wa wawaniaji wa tunzo za Kili Music Awards


Katika hali ya kushangaza na pia ya kupongezwa wana akademi wanaochagua wawaniaji wa tunzo za Kilimanjaro katika hoteli ya Kunduchi Beach Resort, msanii mchekeshaji wa kundi la Ze orijino komedi alitakiwa aondoke kabisa maeneo ya hoteli hiyo ya kitalii baada kubainika kuwa ana wimbo umependekezwa kugombea tunzo hizo mwaka huu huku yeye akiwa mmoja wa wana akademi hao. Baada ya mjadala mkali baina ya BASATA na wana akademi ikaamuliwa Mpoki aondoke kabla  yazoezi hilo kuanza rasmi. Mpoki ana single yake iitwayo Shangazi na imo katika nyimbo zilizo orodheshwa katika kuwania tuzo mwaka huu. Hali hii inaonesha jinsi ambavyo wana akademi wapo makini kuwatambua ama wasanii au ma producer wa video au wa audio ambao wamefanya kazi zinazoshindanishwa mwaka huu wa 2011.
Silvery Mjuni aka Mpoki akiaga wana akademia.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :