Aunt posing with best friend Rehema at Bills Top. With admirer Fatuma Fundikira |
Kwa mujibu wa Anti Ezekiel halisi Mcheza filamu maarufu hapa nchini kuwa hapendi kujihusisha na mtandao maarufu wa kijamii wa FACEBOOK kwa kuwa watu wengi wenye nia mbaya na yeye humuwinda humo, na ili kujiepusha na usumbufu wowote ambao ungeweza kijitokeza ndipo alipoamua kutojiunga na FACEBOOK. Pia Anti amekaririwa na gazeti moja la kidaku akisema kamwe hatojiunga na Mtandao huo kwa kuhofia kuumizwa, ambapo yeye amewashuhudia marafiki zake wakipata wakati mgumu kutokana na kujihusisha kwao na mtandao huo. Lakini hebu jaribu kuingia FACEBOOK na ubofye jina la Ezekiel Aunt utakuta kuna picha kadhaa za Aunt ambazo zinaonesha ni za kuchukuliwa magazetini na pia nyingine zina Alama za Global Publisher ambayo ni kampuni maarufu inayomiliki magazeti ya kidaku yapatayo saba hivi! Hivyo nawaonya wote ambao wangependa kuunda urafiki na Aunt Ezekiel wamtafute kwa njia nyingine na si facebook.
0 comments :
Post a Comment