News
Loading...

Chonde chonde Marekani na washirika wako!


Chonde chonde America na washirika wako msituletee Iraq nyingine ndani ya bara letu la Africa. Sisi wenyewe tuna matatizo kibao yakiwemo ya Zimbabwe, Ivory coast,Somalia na Darfur hivyo hatuhitaji mengine. Nasoma na naona na kusikia Ufaransa imekuwa ya kwanza jana kuwatambua waasi wanaompinga Kanali Moamer Ghadaffi na utawala wake uliodumu kwa miaka 40 na wanampeleka mwakilishi wao mjini Benghazi. Wakati huo huo Hillary Clinton anapanga kukutana na waasi hao ili waseme nini mipango yao baada ya kumuondosha Ghadaffi. Ningekuwa Ghadaffi ningeshafungasha kilicho changu na kutimkia kwa mshkaji wangu Hugo Chaves huko Venezuela, lakini madaraka yalivyo matamu anaona atashinda hii vita ya ndani na kurudi kutawala kama kawaida. Lakini Ghadaffi hajui kuwa anacheza na moto na yatamkuta yaliyomkuta Saddam Hussein. Hawa mabwana wakishaanza kukuundia zengwe la kukutoa madarakani huwa kuna mawili ama wakuue au wakushtaki ICC. Wakati huo huo habari toka Adis Ababa, Ethiopia ambako mkutano wa AU unaokutanisha wakuu wa nchi za Afrika unaendelea zinaeleza AU pia inalaani vikali matumizi ya nguvu ya nayofanywa na majeshi yanayomuunga mkono Ghadaffi, lakini pia hawataki uvamizi wa kijeshi toka nje ya nchi ya Libya kitu ambacho Marekani na washirika wake kinawatoa mate pia habari hizo zimeongeza kuwa AU itaendelea kuyafuatilia maendeleo ya mzozo huo nchini Libya kwa jicho makini.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :