News
Loading...

Breaking news Uso kwa uso na Dada Mage!


Mimi na dada Mage (kati kati)
Baada ya kumaliza kutoa dawa kwa watu waliokwenda kwake tangu saa kumi alfajiri,jioni hii nilipata nafasi ya kumhoji Magreth Mutalemwa (40) mwenye Mume na watoto wanne,na mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo:
Keronyingi- Dada pole na kazi, unaitwa nani?
Magreth- Asante, naitwa Magreth Mutalemwa
Keronyingi- Unaweza ukaniambia pana nini hapa kwako mpaka watu wamejaa kiasi hiki?
Magreth- Mimi hapa natoa huduma ya maji
Keronyingi- Huduma ya maji kivipi?
Magreth- Nawapa watu wanaokuja hapa huduma ya kikombe cha maji
Keronyingi- Ili kiwasaidie nini?
Magreth- Kinawatibu magonjwa wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa mbali mbali
Keronyingi- Ni tangu lini na vipi wewe umejua unaweza kutibu watu?
Magreth- Tangu tarehe 21/March/2011
Keronyingi- Enhe nieleze ilikuaje?
Magreth- Nilikuwa nikipata msukumo baada ya kuoteshwa kabla ya tarehe 21 na kuidharau ndoto ile nilianza kupata matatizo lakini baada ya kuanza kufanya yale niliyotakiwa kufanya matatizo yakaisha ndio mpaka leo natibu watu.
Keronyingi- Dawa yako ina mchanganyiko wa vitu gani?
Magreth- Ni mti mmoja tu, ambao nauchemsha na kuwapa watu wanywe.
Keronyingi- Je umepata kuwasikia watu wengine wanaotoa tiba kama wewe ambao ni Mchungaji Mwasapila, Babu dogo wa Mbeya?
Magreth- Ndio mimewasikia
Keronyingi- Unawazungumziaje?
Magreth- Ah ninavyoona mimi huu ni uwezo wa Mwenyezi Mungu tu, kwani katika uoteshwaji wangu nakumbuka sauti iliniambia tupo watatu na tumetunukiwa  roho safi kufanya shuhuli hii ya kutoa tiba.  Kwa hiyo naamini hao ni wawili na mimi ni wa tatu na ndio tuliotunukiwa.
Keronyingi- Pole kwa kazi na nashukuru sana
Magreth- Asante, karibu tena.
Mpendwa mdau nataraji kuendelea kukuletea habari toka kwa Magreth Mutalemwa mpaka nitakaporejea jijini Dar. Endelea kufutilia maendeleo ya dada na tiba yake toka urban quarter, Uzunguni,Tabora

Foleni ya lala salama kwa leo!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

laiza said...

Yaa Allah utukinge na fitna za masihi dajal....tazama sasa watu walivyogundua namna ya kupata vijisenti vya watanzania. kikombe cha maji tu yaliyochemsha kwa shilingi mia tano.bora imani.
kwa mtindo huu wengi watafurika kupata kikombe lakiniiiiiii...taifa linaelekea wapi jamani.....Mola atupitishie mbali kikombe hichi cha uelekeo wa Kibwetere