Hii ni barabara moja wapo kati ya mbili zinazotoka shule ya Msingi ya Makumbusho kuelekea ile ya Maji machafu, inaonekana inafanyiwa ukarabati sijui wa kiasi gani. Lakini vifusi vinavyowekwa katika barabara hiyo vimekuwa vikimwagikia mferejini na hali hiyo itasababisha maji kushindwa kupita kwa urahisi. Usishangae madongo hayo kubaki humo mpaka mwaka kesho!
0 comments :
Post a Comment