Wakazi wa vijiji vya Kazi kazi na Kitaraka vilivyopo katika kata mpya ya Kitaraka, Jimbo la Manyoni Magharibi, wanalazimika kutembea umbali wa kilometa zipatazo 26 kufuata huduma za ya afya makao makuu ya Tarafa Itigi. Hali hiyo inatokana na vijiji hivyo kukosa zahanati katika kata hiyo ya Kitaraka.Hayo yalisemwa na juzi na Kaimu afisa mtendaji wa kata hiyo, Iddi Manguri wakati akisoma risala yake kwenye sherehe za kumpongeza Mh John Lwanji kwa kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Manyoni Magharibi. Kero kama hizi ndizo zinazoweza kuwafanya wananchi waandamane hasa baada ya kuona magari yanayotumiwa na viongozi kama mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya. Kwa pamoja magari ya hayo huigharimu serikali sh milioni mia tatu na themanini(380,000,000/=) kuyanunua tu, wachilia mbali service zake za kila baada miezi miwili pesa ambazo zinaweza kujenga zahanati na wananchi wa vijiji hivyo wakapata ahueni ya maisha. Lakini je? watu hawa wana uchungu na mwananchi ya kawaida? Hilo ndilo swali la msingi!
0 comments :
Post a Comment