News
Loading...

Breaking News another kikombe Njombe,Iringa!


Dk Anthony Mwandulami
Watu wakingoja kupata vikombe vitatu
Dakta Anthony Mwandulami (58) mkazi wa kijiji cha Itunduma, Wangama, Njombe mkoani Iringa naye amejitokeza kutoa vikombe vitatu vya dawa inayotibu magonjwa kadhaa bila kutoza pesa yoyote kwa sasa. Bw Issa Omari (45) ametoa ushuhuda kuwa dawa ya Dk Mwandulami imemponya Kisukari baada ya kutibiwa kwa muda mrefu katika hospitali za serikali bila mafanikio lakini hali yake ilibadilika ghafla mara baada ya kunywa kikombe cha dawa  Dk Mwandulami ambaye ni mshauri wa watoa tiba asilia wa Tanzania, na juzi Bw Omari alienda kupima katika hospitali ya Ikonda na kuonekana kapona kabisa sukari. Piicha na habari zaidi mcheki Ankal Michuzi.
picha na habari na Francis Godwin

WITO WANGU KWA SERIKALI:
Naafikiri umefika wakati Serikali ichukue jukumu la kuwafuatilia wale wote wanaotoa ushuhuda kujua kama ni kweli wamewahi kutibiwa katika hospitali yeyote ya serikali na kama kweli walikuwa wakiugua ugonjwa husika ili umma wa wa Tanzania uelewe dawa ipi inatibu na ipi haitibu. Sioni kama ni sahihi Serikali kukaa kimya huku vikombe vikichipua kila kona ya nchi hii. Mwingereza anasema "IT IS GETTING RIDICULOUS!" Maana sasa inakuwa kama nchi haina serikali. Watanzania wengi ni wagonjwa na wanataka tiba hasa za magonjwa sugu na hili limethibitika mara baada ya Samunge, Mbeya na Tabora, sasa ni wakati serikali Should stand up and be counted!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :