News
Loading...

Mh Karume na muafaka wa CCM na CUF!


Rais mstaafu Aman Karume.
Siku zote nimekuwa na shaka na muafaka wa CCM na CUF. Mh Karume amesifiwa mno kwa hatua aliyoichukua kuhakikisha muafaka unapatikana. Lakini watu wanaomsifia hawajiulizi kwa nini hakuuharakisha na ukamkuta yeye madarakani? Mimi binafsi nadhani Mh Karume alijiambia "Ngoja nijijengee jina kwenye historia ya Zanzibar" akaupitisha lakini pia akahakikisha kuwa yeye hatokuwepo kushirikiana na CUF.  Serikali za umoja wa kitaifa huwa ni gunia la misumari tu na sidhani kama Mh Karume alitaka kulibeba, akamuachia Mh Shein ahangaike nalo. Kama CUF inataka kuendelea kuishi kwa afya na amani ambapo kwa sasa i mahututi bara itabidi mwaka 2015 wasiingie katika ubia huo tena ambao sidhani kama unawanufaisha wananchi wa kawaida wa Zanzibar. Serikali hiyo ipo kwa ajili ya kupozana, kwa kuwa hutoona Maalim Seif akipigia kelele dawa hakuna hospitali ya mnazi mmoja au serikali ina matumizi mabovu, haiwezekani ng'o! Huwezi ishi kwenye nyumba ya vioo kisha uanzishe vita ya kutupiana mawe.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :