News
Loading...

Mtemi Saidi Fundikira (Sultan Said) 1917-1927


Hili ndilo kaburi la  Mtemi Said Fundikira alizikwa hapo mwaka 1961.

Mtemi Saidi Fundikira (Sultan Said) huyu alikuwa Mtemi maarufu sana katika nchi ya Tanganyika, alitawala kuanzia mwaka 1917 mpaka 1927. Alifanikiwa kuwashawishi watemi wengine  wa kanda ya magharibi kuchanga pesa, mifugo na mali  nyingine ili 
Mtemi Said (sultan said) Fundikira 1956
 kupata pesa za kujenga shule mbili za Tabora Boys na Tabora Girls. Na yeye akatoa ardhi ya kujenga shule hizo kwa kuwa eneo hilo lilikuwa chini ya himaya ya Ikulu ya Unyanyembe. Vile vile Mtemi Said alikuwa mkarimu mno kiasi kwamba mtu akiunguliwa na nyumba yeye alimjengea nyumba mpya na kumpa chakula cha kumtosha kwa mwaka mzima. Na kila mwisho wa mwezi alipokuwa akitoka Bomani kuchukua mshahara wake ulikuwa ni shilingi 4000, ambazo hata Gavana wa Kiingereza Bw Donald Cameron alipata kiasi hicho pia. Watu wenye shida walijpanga katika barabara ya Luhanzali wakimtolea shida zao naye aliwasaidia kwa kuwapa pesa za mshahara wake na hata alipofika Ikulu Itetemia alijikuta kuwa ameishiwa pesa zote. Yeye aliondolewa madarakani na wakoloni wa kiingereza baada ya kuwa hapeleki serikalini kodi aliyotoza wananchi, inasadikika alitumia pesa hizo kusaidia masikini.Yeye alijaaliwa kupata watoto 57 ambao miongoni mwao ndio hawa kina marehemu Chief Abdallah Fundikira, Ramadhani Mlawila(Baba yangu), Kagori biti Said (Mama yake Samuel Sitta) na wengi wengine.Na mpaka sasa katika watoto hao 57 wamebaki wanawake wawili Kagori na Ndisha na mwanamume mmoja Ramadhani Mlawila (87). Ninavyofikiri mimi Sultan Said ndiye aliyeuingiza ukoo huu wa Fundikira katika dini ya ki Islam, kwa kuwa yeye alisomea Zanzibar ambako dini hiyo ilishasambaa huko. Bila shaka aliporudi bara ndipo akaja na dini hiyo ambayo mpaka sasa ndiyo imekua dini ya Ukoo huu. Na hakuna ushahidi kama ukoo huu uliwahi kuwa waumini wa dini yeyote kabla miaka ya 1900. Hivyo basi inaelekea ukoo huu uliabudu mizimu kama ilivyo desturi ya wa Afrika.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

tz biashara said...

Historia nzuri sana, sasa viongozi kama hawa waliojali watu wao watapatikana kweli?Angalia wananchi walivo na shida hivi sasa.Miaka 50 ya uhuru mpaka leo kuna mashule hayana hata madawati,vijijini hakuna umeme wala huko mjini pia mashaka,vijiji havina hata zahanati mpaka watokee wadhamini ndio wasaidie.Sasa nchi iliyokuwa na ardhi kubwa tena ina mimali kibao lakini bado hatujajaaliwa kumpata kiongozi ambae mwenyekujua kuikuza nchi kwa kugawa elimu ambayo ndio itakayo endeleza vizazi vijavo.