News
Loading...

Pakistani inapowakatalia Marekani kumhoji mke wa Bin Laden!


Sheikh Osama Bin Laden.
Maofisa usalama wa Pakistani wameikatalia Marekani kumhoji mke mdogo wa Bin Laden aliyejeruhiwa wakati wa mauaji ya Osama yalipofanyika. Maofisa hao ambao bado wamenuna juu ya Marekani kuingia angani mwao bila taarifa na kumuua Bin Laden pia bila kushauriana nao, wamewajibu Marekani jana baada ya kutaka Pakistan iwakabidhi mke huyo wa Osama Amai Abdulfattah(27) ili wamhoji, Pakistan imesema atakabidhiwa kwa nchi yake ya Yemen mara atakapopata nafuu katika hospitali ya jeshi la Pakistani mjini Rawalpindi ambako anatibiwa majeraha yake.

Msemaji wa idara ya mambo ya masuala kimataifa wa Pakistan alisema " Serikali ya Pakistan ina mashaka makubwa kwa jinsi America ilivyolishuhulikia suala hili na kumuua Bin Laden bila sisi kuhusishwa"

Na katika kuongeza chumvi katika kidonda cha Pakistan mkurugenzi wa CIA Leon Panetta alisema "iliamuliwa kuwa jitihada zozote za kuihusisha Pakistan ungehatarisha mpango mzima, kwani wangeweza kumshtua Bin Laden na akatoroka kabla ya kuvamiwa"

Mataifa ya Magharibi na Marekani yamekuwa katika tahadhari kubwa mara baada ya kifo cha Osama Bin Laden, yakionya kifo hicho hakitokuwa mwisho wa falsafa zake bali mwanzo wa mashambulizi ya kisasi ya kustukiza bila maonyo.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :