Leo hii nilisikiliza kipindi cha michezo cha Sports Extra kinachorushwa na 88.4 Clouds Fm nikasikia kuwa CAF wameupitisha mji wa Cairo kuwa ndio mji utakaotumika kuchezewa mchezo wa Champions League ya Africa kati ya Simba Sports Club ya Tanzania na Wydad Cassablanca ya Morocco. Timu hizo mbili zitakutana baada ya TP Mazembe kuondolewa mashindanoni na CAF baada ya Simba kuikatia rufaa TP Mazembe baada ya kuituhumu kuwa ilimtumia mchezaji ambaye alikuwa hajamaliza mkataba na timu ya Esperance ya Tunisia. Baada ya uCAF kufanya uchunguzi tuhuma za Simba zikabainisha kuwa ni kweli ndipo Mazembe wakondolewa mashindanoni.
Lakini mimi naona kama CAF hawakuwa sahihi kuichagua Cairo kuwa ndio neutral ground ya kuchezewa mchezo huo, kwa mtazamo wangu Wydad watajisikia nyumbani zaidi ya Simba ukiondoa uwezo wao mkubwa wa kucheza mpira kuliko Simba. Kama CAF wanaona hilo halina utata kwa nini wasingeichagua Nairobi kuwa mwenyeji wa mchezo huo? Ingekuwa vema mchezo huo ungechezwa Luanda, Angola ambako pasingekuwa na timu yeyote ingesema wenzao wana ka adgvantage kadooogo! ka Lugha mdauu!
0 comments :
Post a Comment