News
Loading...

Ya simba SC yanaweza itokea Man united pia!


WASI WASI; Sir Alex Ferguson meneja wa Manchester United.
Mwaka huu tumeshuhudia Yanga Afrika ikiipiku Simba Sports kutwaa ubingwa wa Tanzania kwa tofauti ya goli moja tu, na hili laweza itokea Man united. Kuna wakati Simba iliongoza ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya huduma ya simu za mkononi Vodacom kwa tofauti ya pointi tisa. Lakini hatimaye wakaukosa ubingwa kabisa. Na hili liliwezekanaje? Ni juhudi ya viongozi, kocha na wachezaji kutokata tamaa n a kuendelea kuamini kuwa iwapo Simba wangetetereka wao wangekuwepo kuwapiku na ndicho kilichotokea. Sasa nahisi hilo laweza tokea katika EPL. Man u kuna wakati wameongoza hasa dhidi ya Chelsea kwa pointi 15 hivi, lakini leo Man united haina uhakika wa kuchukua ubingwa huku zikiwa zimesalia mechi mbili kwa kila timu pia mchezo mmoja utakuwa kati ya timu hizo mbili Chelsea dhidi ya Manchester United. Hesabu ni nyepesi kwa Man united nayo ni lazima waifunge Chelsea kisha wabakiwe na mchezo mmoja dhidi ya Blackburn Rovers ambao wakiwa katika hali ya kimchezo wataishinda tu, lakini hiyo pia ni moja ya zile mechi ngumu (tricky) ambazo huwezi kuweka nyumba yako rehani kwa matokeo yake.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :