News
Loading...

Lifti ya Shoppers Plaza mtihani!


Lifti hii isiyo na kiyoyozi ni hatari kwa watumiaji
Je mdau umepata tumia lifti ya Shoppers Plaza ambayo hukufikisha katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo? Lifti hiyo ambayo haina kiyoyozi cha aina yeyote na pia imezungushiwa urembo wa vioo vizito ambavyo havina uwazi (vent) ya aina yeyote ni htari sana kwa watumiaji hasa wale wenye shinikizo la damu, kwani humo kuna joto kali ambalo ukiondoa ukosefu wa hewa ndani humo pia lifti hiyo humulikwa na jua kuanzia asubuhi mpaka mchana hivyo kusababisha iwe na joto mara mbili ya lile la kawaida. Sijawahi kusikia kama pana idara ya afya na usalama (Health & Safety) hapa Tanzania lakini nina hakika ingekuwa nchi zilizoendelea wamiliki wa jengo hilo wasingeruhusiwa kuitumia lifti hiyo hasa nyakati za mchana. Lakini ndio hivyo sasa, ndio kwanza nchi ina miaka 50 ya umri tusubiri tukue kidogo!
Shoppers Plaza inavyoonekana kwa nje

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :