News
Loading...

Tabora yachanua Miss Kanda ya kati! Flora Michael ashindwa kuendeleza ubabe wa Tabora!


Maua Kimambo mshindi wa pili Miss kanda.

Dalilah Gharib mshindi wa Tatu.

Florah Michael akosa nafasi.
Baada ya kusota kwa zaidi ya miaka kadhaa bila mafanikio hatimaye mkoa wa Tabora usiku wa jana kuamkia leo katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma ulifanikiwa kupeleka warembo wawili Miss Tanzania kwa mwaka wa pili mfululizo kwani mwaka jana Tabora iliwakilishwa Miss Tanzania na Pili Issa Miss Tabora 2010. Kwa bahati mbaya mwaka huu Miss Tabora 2011 Flora Michael alishindwa kuendeleza ubabe wake wa Tabora baada ya kukosa nafasi ya kwenda Miss Tanzania pamoja na kuwa aliingia katika top 5. Shindano la Miss kanda ya kati ambalo hujumuisha warembo 12 jumla, watatu toka toka Kigoma, watatu Singida, watatu Tabora na  watatu Dodoma ambao ndio wenyeji. Mshindi wa kwanza Miss Zeulia John alitoka Dodoma akifuatiwa na Maua Kimambo wa Musoma utalii college na Dalilah Gharib wa Uhazili (TPSC) wote toka Tabora. Maua na Dalilah walikuwa washindi wa pili na wa tatu katika Miss Tabora. Lakini Dodoma wameweza kupita kwenda Miss Tanzania huku mbabe wao akikosa nafasi hiyo katika shindano lililotawaliwa sana na warembo wa Tabora. Hongera muandaaji wa Miss Tabora kwa kuutoa mkoa kimaso maso.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :