News
Loading...

Muandaaji wa Miss Tabora atamba warembo wake kuitingisha Miss Tanzania 2011


Toka kushoto Florah Michael, Dalilah Gharib na Maua Kimambo
CONFIDENT: Mgalula Fundikira.
Muandaaji wa Miss Tabora Bw Mgalula Fundikira ametamba kuwa warembo wake wawili waliopita kwenda Miss Tanzania Maua Kimambo na Dalilah Gharib watafanya makubwa katika shindano la Miss Tanzania, litakalofanyika jijini Dar baadae mwezi ujao. Mgalula ameandika katika ukurasa wake wa Facebook akiwataka warembo watakaopita kwenda miss Tanzania toka kanda nyingine wakae chonjo. Pia amewashukuru suppoters na staff wote wa Club Royal Entertainment na wakazi wa Tabora ambao walisaidia kutafuta warembo hao.pia amesisitiza alichokiongea katika runinga ya TBC1 alipohojiwa na Niko Mwibale mara baada ya Miss Tabora kupatikana tarehe 27/05/2011 ambapo alisema "washiriki wengine wa miss kanda ya kati wakae chonjo kwani warembo wake wataenda Dodoma kukamilisha ratiba tu kwani kwa ubora wao anatarajia taji la Miss Tanzania litue Tabora kwa mara ya kwanza tangu shindano hilo maarufu lianzishwe hapa nchini. Mimi binafsi nawatakia kila heri warembo Maua Kmambo na Dalilah gharib wakatutoe kimasomaso wana Tabora.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :