News
Loading...

Mzee Yusuf apagawisha Tabora!




Mzee Yusuf akiimba moja ya nyimbo zake.
Wapenzi wa taarab wakikongeka nyoyo jana.
Waimbaji wa Jahazi Modern Taarab
 Jana usiku katika ukumbi wa Frankman Palace mjini Tabora Mzee Yusuf pamoja na kundi lake  Jahazi Modern Taarab waliporomosha show ya aina yake, show hiyo iliyovuta watu takriban mia sita hivi ilihudhuriwa pia na Mkuu wa wilaya ya Uyui Bw Mosi Chang'a iliwakonga nyoyo wapenzi wa muziki huo wa mwambao hasa pale Mzee Yusuf alipopanda jukwaani kutumbuiza. Nguli huyo wa taarab alisababisha fujo kubwa ya washabiki wake kila mmoja kutaka kupiga naye picha au kumshika mkono, mpaka pale mwenyewe alipowaomba wapande jukwaani kwa zamu. Mzee Yusuf amekuwa akipendwa sana mjini hapa kwani mara ya mwisho kuja Tabora  mwaka juzi alipozuru mkoa huu mashabiki wake walijaa mno katika ukumbi wa New Royal Garden. Baada ya Tabora Jahazi modern Taarab leo usiku watatumbuiza Kahama na kisha Shinyanga siku ya jumamosi.
Wapenzi wa taarab Tabora
Mimi na Mgalula Fundikira wa club royal Tabora

Mimi na mfalme wa Taarab Mzee Yusuf

Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Uyui Mh Mosi Chang'a kushoto

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :