News
Loading...

Hatimae Yanga yagoma kuvaa jezi zenye nembo ya vodacom ambaye ndiye mdhamini wa Tanzania premier league


Timu ya Yanga Afrika ya jijini Dar imekataa rasmi kuvaa jezi zenye nembo mpya ya mdhamini wa ligi kuu ya Tanzania ijulikanayo kama Vodacom Premier League.Yanga ambao walishatahadharisha mapema kuwa wasingevaa jezi zenye nembo hiyo mpya ya Vodacom. Yanga hii pia inaongozwa na mwanasheria wa kujitegemea Bw Loyd Nchunga lakini katika suala la rangi ya nembo ya vodacom ameamua kuweka taaluma yake pembeni na kuanzisha ubisha wa kishabiki (USIMBA YANGA). Lakini kwa nini tumshangae kiongozi wa klabu ya Yanga kwa kuingoza timu yake isivae jezi hizo, wakati tumeona vilabu hivi vikongwe kila vikipoteza mchezo dhidi ya mojawapo huwageukia wachezaji na kudai kuwa wamehujumu mechi? 
Lloyd Nchunga akipokea jezi toka Tbl .

Kwa kumalizia tu nafikiri ni jukumu la TFF kuhakikisha wanalishuhulikia suala hili ipasavyo ili lisijirudie tena, kwani vitendo kama hivi vitapelekea kuwavunja Moyo wadhamini hasa ukizingatia vilabu hivi vinahitaji sana dhamini hizi ambazo ndizo chacxhu za maendeleo ya soka hasa nchni mwetu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :