News
Loading...

Wabunge wa Zanzibar walipomjia juu Tundu Lissu


Mh Muhammad Chombo
Baada ya Wabunge wa Zanzibar kumjia juu waziri kivuli wa sheria wa kambi ya upinzanzani Mh Tundu Lissu baada ya hotuba yake, mbunge wa Magomeni Mh Muhamad Chombo alitia fora kwa kusema "Napenda kumfahamisha yeye (Lissu) pamoja na wengi humu ndani (Bungeni) na wale walio nje ya jumba hili wenye mawazo mgando kama yeye, Zanzibar si koloni la Tanganyika na hata siku moja halitokuja kuwa koloni la Tanganyika. Na Mh Lissu agosti nane alizungumza mambo kuhusu muungano akajaribu kuwataja viongozi waathirika wa muungano, ambapo nimuongo na mnafiki"  

Kauli kali kama hizi zitakuja epukwa tu siku za mbeleni kama, ama tutakuwa na serikali moja au tatu ili kuondoa malalamiko toka pande zoter za muungano ambao ni dhahiri umekuwa wa viongozi badala ya kuwa wa wananchi. Pia nafikiri itakuwa vema pawe na mkutano wa kutunga katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambao utaondoa dosari zote zilizomo katika muungano huu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :