News
Loading...

Sakata la Jairo, kwa nini Ngeleja na Malima bado wapo kazini?


Vigogo wa Madini na Nishati.
Baada ya waraka wa Bw David Jairo kwenda kwa taasisi kadhaa zilizo chini ya wizara ya Nishati na Madini kuzitaka kuchangia milioni 50 kila moja ili kuchangia upitishwaji wa bajeti ya wizara hiyo ya 2011/12 kuleta kizaa zaa bungeni na hatimae kupelekea kusimamishwa kwa katibu huyo wa wizara hiyo nyeti. Kinachonishangaza mimi ni kuwa kama Jairo alisimamishwa kazi kwa tuhuma za rushwa kwa nini mabosi zake hawakusimamishwa pia? Inawezekana kitu kama hicho kilifanywa na Jairo bila waziri na naibu wake kujua? Absolutelly impossible. Bado tupo kule kule "Kulindana" na "saving face". Jairo ametolewa kafara. 
Shangwe za kumpokea Jairo
 Naye Jairo mwenyewe au sijui ni nani katika wizara hiyo aliyeandaa kumpokea Bw Jairo kwa mapokezi ya kishujaa kurudi ofisini, kwa mtazamo wangu lilikuwa ni jambo la kijinga kidogo kufanya. Kana kwamba haitoshi Jairo akasikika akisema runingani kuwa yeye hatowashitaki waliosababibisha asimamishwe kazi na amewasamehe kwani hataki kulipa kisasi. Sasa mimi najiuliza kwani si kweli kuwa Bw Jairo alichangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti ya wizara yake? Sasa basi anawasamehe vipi wakati yeye katenda kitendo hicho?

Nafikiri pia Bw Luhanjo katibu mkuu kiongozi aliyemrudisha Jairo kazini na kumsafisha pia kakalia kuti kavu, tusubiri tuone baada ya uchunguzi wa Kamati rasmi ya Bunge.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :