Nembo ya Simba sports club |
Kwa kilabu chenye ukubwa wa Simba sports club ni aibu kuwa na nembo (crest) ya bei rahisi kama hiyo hapo juu kwani haiendani na ukubwa, umaarufu,utajirina vingi ambavyo nikivitaja havitoisha leo. Pengine uongozi wa Simba unafikiri kwa kuwa kilabu hichokinaitwa Simba basi ni lazima mnyama simba awepo katika hali hiyo anayoonekana hapo juu, nadhani angeweza kuwa hata kama simba huyu hapa wa Lyon ya Ufaransa.
Ukitazama kwa umakini hata nembo ya Azam tu inatazamika vema kuliko huyo Simba mnyama aliyepo katika nembo ya Simba sports club tazama nembo ya Azam hapo chini ni nzuri na inapendeza.
Natumai viongozi wa Simba watakuwa wameliona hili na watalifanyia kazi ili timu hiyo iwe na nembo stahiki.
0 comments :
Post a Comment