News
Loading...

Bilioni kumi hadi ishirini ni kitu gani kwa serikali?
Daraja kama hili litapunguza msongamano Tabata/Kigogo
Kwa mtazamo wangu wa ki mbu mbu mbu naona ipo haja serikali ijenge daraja (Bypass) katika maunganiko ya bara bara itokayo kigogo kwenda Tabata (Sheli) na Br ya Mandela. Nikizingatia daraja hilo litaigharimu serikali kiasi kidogo cha sh 5 bilioni kulijenga na pengine na mpaka sh 20 bilioni ikiwa ni pamoja na kulipa fidia wakazi wa maeneo hayo watakaovunjiwa nyumba zao. Hili jambo linaweza kufanyika kama serikali itaamua kulifanyia kazi na faida zake zitaonekana wazi kwa kupunguza msongamano wa magari nyakati za asubuhi na jioni, nafikiri wakazi wengi wa eneo hilo watakubaliana na wazo hili kwani watu watokao mjini kwenda Tabata na Segerea kwa kupitia njia ya Kigogo watakuwa wanapita juu ya daraja hilo badala ya ilivyo sasa ambapo hulazimika kuingia katika msongamano wa Mandela Rd.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :