Mh Tibaijuka: Anahitajika Msisiri |
Waziri wa ardhi Mh Anne Tibaijuka amefuta hati 42 za viwanja vilivyopo katika maeneo ya wazi jijini Dar hasa katika wilaya ya Kinondoni. Huu ni muendelezo katika vita yake dhidi wajenzi holela jijini Dar. Bado najiuliza itakuwaje akifikisha vita yake maeneo ya Mwananyamala Msisiri ambako chama tawala kimejitwalia maeneo kadhaa ya wazi na kuweka ofisi zao huku wenye hati halali katika maeneo hayo wakiathirika kwa kushindwa kuingiza gari zao ndani ya nyua (fence), pia kuwa katika hali hatarishi iwapo patatokea ja
nga la moto katika maeneo hayo kwani gari za kuzima moto hazitoweza kuzikaribia nyumba hizo. Mimi ningependa tu afike Msisiri na awaondolee kero wakazi wa mtaa wa Gulwe.
0 comments :
Post a Comment