Ashley Young |
Chama cha soka cha England (FA) Kimelilalamikia shirikisho la mpira wa miguu la nchi za Ulaya UEFA pamoja na Chama cha soka cha Bulgaria baada ya baadhi ya mashabiki wa Bulgaria kuwadhihaki kibaguzi wachezaji weusi wa England akiwemo Ashley Young. Washabiki hao walikuwa wakiiga milio ya nyani na kufanya saluti ya kinazi iliyotumiwa na Dikteta wa Kijerumani Hitler na wafuasi wake, adha hiyo ilitokea pale England ilipopambana na Bulgaria na kuifunga timi bao 3-0.
Shujaa wa magoli mawili ya England Wayne Rooney alisema kwa hasira "tulisikia wazi wazi walichokuwa wakisema,jambo hili limekuwa likiendelea kwa muda mrefu na si sawa. Umefika muda sasa jambo hili lifikie mwisho na natumai kuna hatua zitachukuliwa"
Kocha wa Bulgaria Lothar Matthaus ameomba msamaha kwa tukio hilo akisema "Ni jambo la kusikitisha kutokea".
mchezaji wa Arsenal Theo Walcott alisema " nilisikia wazi wazi lakini nilipuuzia tu, lakini kwangu kitu muhimu ni pointi tatu tulizopata" Walcot alikuwa mmoja wa wachezaji weusi waliodhihakiwa kibaguzi jijini Sofia katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za ulaya mwaka 2012. Msemaji wa FA alisema "Tumewafahamisha chama cha soka cha Bulgaria na shilikisho letu UEFA
0 comments :
Post a Comment