News
Loading...

Akipatikana na hatia John Terry avuliwe unahodha, na si wa England tu na Chelsea pia


John Terry

Anton Ferdinand
Baada ya FA na polisi wa jijini London kumchunguza John Terry baada ya kamera kumuonesha akimtusi Anton Ferdinand kibaguzi na picha mwendo hizo kuwekwa katika mtandao wa Youtube, pale Chelsea ilipocheza na Queens Park Rangers  pia ya London, kumekuwa na kauli nyingi zimetolewa hasa na wachezaji weusi wa zamani huku binamu yake Anton Ferdinand, Sir Les Ferdinand akipendekeza John Terry akipatikana na hatia anyimwe kuichezea tena England wachilia mbali kumvua unahodha wa timu hiyo ya taifa. Watu kadhaa maarufu wameoneshwa kustushwa na kashfa za kibaguzi zilizoikumba Premier League hivi karibuni. Sir Alex Ferguson alisema "nimeshangazwa sana na sikutegemea mwaka 2011 nisikie wachezaji wanatukanwa kibaguzi. Patrice Evra wa Man united pia amemtuhumu  Louis Suares wa Liverpool
kumtusi kibagu kwa kumwita Negro zaidi ya mara kumi siku timu zao zilipopambana katika uwanja wa Anfield jijini Liverpool wiki 2 zilizopita na kashfa hiyo inachunguzwa na FA.


Mtazamo wangu ni kuwa itakuwa fundisho kwa wengine kama Terry atafukuzwa kuichezea England na Chelsea wampoke unahodha iwapo atapatikana na hatia. Yote na yote nashindwa kuamini kuwa John Terry ni mbaguzi ingawa ametumia lugha ya kibaguzi katika kesi hii.

Les Ferdinand

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Anonymous said...

Kaka mbona wewe unashabikia ubaguzi wa Terry juu ya rangi, vipi na wewe na udini wako?