News
Loading...

Uingereza isiziyumbishe nchi za Afrika kwa kigezo cha demokrasia ya ushoga


Ushoga oyeee!

Duh patachimbika!
Kauli ya waziri mkuu wa Uingereza Bw David Cameron wakati akifunga mkutano wa jumuia ya madola mjini Perth nchini Australia ya kutishia kutozisaidia nchi zisizounga mkono suala zima la ushoga (Homosexuality) na ndoa za jinsia moja (Gay mariages) inaonesha jinsi gani watu hawa (Europeans) walivyo ndumi la kuwili (Hypocrites). Waingereza wao ndio vinara wa demokrasia duniani, lakini wanataka kuzilazimisha nchi masikini (Afrika) kuunga mkono mambo ambayo hayana nafasi katika jamii zetu wala hayajawahi kuwa na nafasi. Demokrasia ya kweli ni pale watu wanapoachiwa kujiamulia mambo yao wenyewe, sisi Tanzania tumeamua ushoga hauna nafasi katika katiba yetu. Kwa nini watuamulie nini cha kufanya kama wao ni wapenda demokrasia? Ukweli usiopingika ni kuwa Tanzania haiwezi kupelekwa pelekwa kishoga. Hii inaashiria tupo karibuni mno na mwisho wa dunia kwani dalili zote zinaonesha hivyo! Rais wa Zimbabwe Mh Robert Mugabe aliliona hilo mapema pale alipomshukia waziri mkuu wa Uingereza wakati huo Bw Tony Blair na kuiita Uingereza UNITED KINGDOM OF GAYS.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

Kaka ni wewe ndio umeandika hii habari au ume copy and ku paste? sababu umesema "suala zima la ushoga" kwenye mabano umesema (bisexuals)...nadhani kuna makosa hapo...bisexuals ni mtu ambaye anakuwa yupo attracted for both kama ni mwanamke basi anakuwa attracted kwa mwanamke pia wanaume....na kwa mwanaume ni hivyo pia. Ushoga kwa hujumla ni homosexual....ni correction tu. Nashukuru pia kwa habari za Matipa, namfahamu sana, mimi nimekulia Bachu.

Mdau
Canada

Mkala Fun said...

Nimeandika mimi baada ya kuibuka issue hiyo,asante kwa marekebisho. I dont know why i used that word there. Kuhusu Matipa its sad that he left us so in that age! Mungu amrehemu!