News
Loading...

Amerika itapigania haki za mashoga katika nchi za kigeni-Clinton


Bibi Hillary Clinton.
Marekani imetamka wazi wazi kuwa itapigania haki za mashoga na wale wanaowapenda kimapenzi watu wa jinsia zao. Clinton alikuwa akiongea na mabalozi wa nchi tofauti mjini Geneva, Clinton alisema "Isiwe ni kinyume cha sheria kuwa shoga" Akaongeza "Tamaduni na dini zisitumike kama visingizio vya kuwadhalilsha mashoga" Katika mabalozi aliowahutubia walikuwemo kutoka nchi ambazo zimepiga marufuku vitendo vya kishoga nchini mwao. Bibi Clinton akaendelea "Ushoga si kitu cha kujitakia, wamezaliwa katika jumuiya zetu pia ushoga si tengenezo la nchi za magharibi bali ni uhalisia wa mwana Adam" Mabalozi wengi waliwahi kutoka ukumbini haraka mara Clinton alipomaliza hotuba yake. Saudia Arabia, Afghanistan, Ghana, Uganda na Nigeria ni kati ya nchi ambazo zimepiga marufuku ushoga wa aina yeyote ule.


Miezi kadha iliyopita wa Tanzania wengi walijazibishwa mno na maneno ya waziri mkuu wa England Bw David Cameron kuwa Uk haitazisaidia nchi zitakazopinga ushoga hata hivyo kauli hiyo ilikanushwa vikali na Afisa wa wizara ya mambo ya nje wa Uk ambaye alidai wataendelea kuisaidia Tanzania na wataheshimu tamaduni zetu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Anonymous said...

Habari za Dar? sasa kaka wewe unasema kwa hilo, je unapinga? Mimi binafsi nadhani kwa utamaduni wetu hili swala ni gumu sana kulielewa even kuvumilia. Lakini je, kama kuna ndugu yako anakwambia kuwa ni gay, je unaweza kumtenga au? mimi nadhani hawa watu wa West wasifanye nguvu kutulazimisha kwa hili, mimi ningeona ni bora wangesema haki za binadamu lakini siyo kulazimisha kuwa kwa sababu huku West ni okay basi na sisi tufuate. Hata hapa West...kuna watu bado wanapinga sana suala hili...at the end ni lazima ukubali kuwa hawa magay ni watu ambao wanaishi na sisi, unafanya nao kazi nk.
Mdau
Canada

Mkala26 said...

Mimi napinga ofcoz lakini ni position ngumu sana tunakuwa ndani yake, kama mfano ulioutoa wa ndugu yako anakwambia yeye ni shoga utamtenga? Hapana huwezi, nafikiri so far we are doing well here in Tz concerning that issue, coz we all know we do have gays and lesbians but we jus carry on live with them without any problem. Sijui sheria ya nchi inasemaje kuhusu hilo lakini may be we shud stick to what we have. Asante kwa maoni.

tz biashara said...

Hamna lolote hawa watu wasitulazimishe ktk tamaduni zao.Wanazungumzia masuala ya haki wakati hawatimizi haki za kibinaadamu ktk nchi za watu wanavoua kama kuku.Halafu mtu huyu aje akwambie mambo ya kishetani yapewe haki.Jamani hii ni karne nyingine kabisa na sio ya kutawaliwa tena.Wanahangaika na uchumi wao kwahio wanatafuta pa kuingilia hasa huku Afrika wameshaipata Libya sasa wanasogea East Africa.Sasa hawajui wataingia na gia ipi kwahiyo wankuja na njia ya kuja kuwakomboa mashoga.Nisawa na kuwafundisha watoto wetu ili waambiwe wachague maisha gani wanataka kuishi na ndivo ilivo huko kwao.Imagine mtoto mdogo wa miaka 6 au 7 kama sikosei wanaanza kuwafundisha somo la "sex education"na wanaambiwa ukitaka kuwa gay ni chaguo lako na asilazimishwe mtoto na ukimfanyia fujo serikali inamchukua na kumlea.Na malezi atakayopewa huko ni free vile atakavo.Sasa hapo mtoto akipotea watasema ndio maisha alioyachagua.Angalia kesi ya mapadri wa katoliki ambao wamewafanyia uchafu watoto wakiume na wakike mpaka leo kesi hazijaenda mbele na kuhukumu.Na hawa watu wengi wao hivi sasa ni watu wazima wengine wameoa na wengine hawajafanikiwa kuo au kuolewa.Na mashoga wengi historia zao ni za kubakwa utotoni kwahiyo pia wanayashabikia hayo au kumuonea huruma mtu huyu.Je mbona hatuwaoni watoto wao kuingia ktk mambo hayo au wakwao ni special au ndio ile methali ya mkuki kwa nguruwe lakini kwa binaadamu ni mchungu.