News
Loading...

Kwa nini kampuni za kutengeza pombe haziruhusiwi kudhamini matamasha zanzibar?


Wachezaji wa Simba wakiwa wamevalia jezi zenye alama
 ya bia ya kilimanjaro  ambao ndio wadhamini wa klabu hiyo.
Wapenda wadau leo hii nilitokea kujadili na washikaji suala la kwa nini kampuni za pombe haziruhusiwi kudhamini matamasha, ligi za michezo mbali mbali nchini Zanzibar? Ilihali pombe zinauzwa huko na pia hao walioweka sheria hizo wao ndio vinara wa kutumia vilevi. Sasa hapo naona kuna hali ya kuchagua dhambi, "nguruwe haramu, lakini mchuzi wake twaunywa yakhee! 


Na pia ukitazama kwa makini hivi sasa huku bara vilabu vya Simba na Yanga vinadhaminiwa na TBL kwa mikataba mizuri tu, pia  TBL imekuwa ikidhamini matamasha mengi ya muziki na michezo. Kwa kifupi katika nyanja hiyo bara mambo ni mazuri sana. Nafikiri umefika wakati viongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar waliangalie hilo vizuri, ili waruhusu kampuni hizo zidhamini matamasha ambapo viwango vya timu za mpira wa miguu vitapanda sana ukilinganisha na sasa. Haya ni maoni yangu tu!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

WAO KAMA WAMEAMUA HIVYO NI SAWA,KAMA SUALA LA KUPATA PESA KUNA MAMBO MENGI YANAWEZA KUFANYWA NA MAPENE YAKAPATIKA,,, NI SUPPORT WASIRUHUSU KWASABABU HAYO MAPOMBE YANAHARIBU MAISHA YA WATU WENGI ILA SISI( KWA MAONI YANGU) TUMEKUWA HATUANGALII MADHARA YAKE TUNACHOANGALIA MAPESA TUU,,FANYA UTAFITI ANGALIA KWENYE MEDICAL JOURNALS UTAONA POMBE INA NINI.. AFTRE ALL NI MAAMUZI TU YA JAMII KAMA VILE WATZ HATUTAKI USHOGA UHALALISHWE BASI JAMAA WANATUSHANGAA KWELI,,,,KAMA HAWATAKI BASI

Anonymous said...

Mkala siku nyingi sijaingia ktk Blog yako nauhakika unaendelea vizuri kimaisha.Ama ktk hili suala Mkala itabidi nikupinge sana na sio kidogo.Kama alivosema mdau alie tangulia ni kweli hapa kwetu Bongo sisi tunaangalia suala la pesa tu lakini hatupendi kuangalia pesa yetu inaingia kupitia wapi.

Tusiwalazimishe Zanzibar kukubali kudhaminiwa na kampuni za pombe.Pombe kama tunavojuwa ni haramu kwa waisilamu na unafahamu fika kama Zanzibar ni nchi tulioungana nao na idadi ya waisilamu ni 99%.Sijawahi kumuona mzanzibari hata mmoja anaeshabikia pombe ktk nchi yao isipokuwa wageni ndio waliosababisha kuuzwa kwa pombe kwa wingi hivi sasa.Haimaanishi kwamba mnywaji pombe akubali kuuza au kuitangazia.Pombe inamadhara makubwa kuliko faida.Kwanini usizungumzie kampuni nyingine kuliko pombe.Nadhani nyinyi watu wa Blog ni muhimu kutoa masomo muhimu ya kiafya na maisha bora kuliko kupigia debe mambo yenye kusababisha "crimes,violence,rape,maambukizi ya maradhi ya ngono,umasikini na mengi tu maana hatuwezi kuyamaliza.Haiwi hata ulaya wenye kutengeneza kwa wingi na wanywaji wengi hupiga kelele ya kutotangaza ktk TV kwasababu wananchi wao wengi wanapoteza maisha kwa kutumia pombe kupiliza kiasi.Wanazo mpaka program za kuwaonyesha wananchi kuhusu madhara ya pombe kiafya.Angalia dada zetu na kaka zetu leo hii wanavobugia pombe mpaka wanafanya maajabu.