News
Loading...

Open space yavamiwa na kuegeshwa magari usiku


Hili ndilo eneo linalolalamikiwa ubavuni mwa nyumba ya
kada wa CCM Mzee Mohamed hapo Msufini.
Wakazi wa Mtaa wa Guta, Kinondoni, Msufini wamelalamikia kitendo cha watu wasiofahamika kuanzisha biashara ya kugesha magari mbele ya nyumba zao, jambo ambalo linaweza kuleta madhara iwapo patakuwa na mgonjwa ambaye hawezi kutembea lakini anahitaji gari ifike mlangoni kwake ili afikishwe hospitalini, na hilo likitokea usiku mwingi hunenda mgonjwa huyo akakosa hata watu wa kumbeba na kumpeleka katika gari. Kwa jinsi ninavyofahamu mimi maeneo ya wazi kama haya huweza kutumika kwa huduma za kijamii tu na si biashara ya kuegesha magari na vile vile wakazi wa eneo husika lazima waitwe katika kikao na viongozi wa serikali ya mtaa kuwashauri juu ya jambo hilo.  Madhara mengine yanayoweza kutokea katika maeneo hayo ni pamoja kuanzisdha kwa gereji bubu katika eneo ambapo hupelekea usumbufu kwa wakazi na jamii kwa ujumla.


Nilipomuuliza mlalamikaji mmojawapo ni hatua gani wamechukua baada ya uvamizi huo? Amesema kuwa wapo katika harakati za kushauriana kisha watawaandikia barua Diwani wa kata ya Mwana nyamala na Mbunge wa jimbo la Kinondoni ili kueleza malalamiko
yao huko.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

fatma said...

kwa kweli inakera sana hasa pakijaa magari mpaka mlangoni mwa gati letu