News
Loading...

Hali hii itaendelea mpaka lini?


Hali ilivyo maeneo ya jangwani.
Napenda kuelekeza swali langu kwa serikali na idara zake zote husika. Matukio ya mafuriko mwaka huu katika maeneo ya mabondeni si ya kwanza na wala si ya mwisho, tumeona hasara nyingi zikitokea miaka nenda miaka rudi na tumshuhudia wananchi wakipoteza maisha katika matukio haya huku ya mwaka huu yakivunja rekodi kwa watu zaidi ya 40 kupoteza maisha (BBC). Sasa nashangaa na kubaki najiuliza je? kuna kitakachofanyika kuhakikisha janga hili la mvua kubwa litakapokuja tena halitokuta wananchi katika maeneo hayo? Jibu la swali langu wanalo mabwana wakubwa serikalini, kwa sababu watu hao wasingejenga huko mabondeni sama na wao serikali kuwaachia wajenge huko huku wakijua fika eno hilo ni hatari ikitokea mvua kubwa. Lakini kwa uchu wa vijisenti wakawapa huduma zote muhimu ikiwamo maji na umeme pengine walipewa hata leseni za makazi (mfano wa hati ya nyumba). Fanyeni mfanyalo muwahamishe hao watu huko mabondeni kama pesa mnazo nyingi tu kwa kutaja chache kuna za EPA na zile za Mzee wa Vijisenti yaani CHENJI YA RADA.
PICHA KWA HISANI YA BILAL AHMED

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Mzee wa Changamoto said...

Yataendelea mpaka sisi (WANANCHI) tutakapoamka na KUSITISHA

tz biashara said...

Mkala inabidi ufahamu kwamba sisi wananchi tunayo makosa makubwa kwa kuendekeza umasikini.Hao wananchi waliojenga walijua waziwazi hawaruhusiwi kujenga lakini walijenga kwa makusudi.

Wakulaumiwa zaidi ni wafanyakazi wa serikali za mitaa.Kwa njaa zao wanaangalia watu wanajenga mpaka wanamaliza na kuishi kwa muda mrefu.Na pengine hutoa taarifa kwa wanaohusika lakini hawataki au ni wavivu kuwajibika.

Lakini vilevile waliwahi kuambiwa wahame wakati wa mafuriko miaka ya nyuma,na wakapewa viwanja lakini matokeo yake wengi walirudi mabondeni na viwanja wakauza.

Na kingine Mkala hawa wanasiasa wetu hujituma kwa kura tu kwasababu haya mambo yanavotokea wao hujitafutia kura.Kwanini nasema hivi,wakiambiwa wahame mabondeni basi wanasiasa huja juu na kusema wananchi wananyanyaswa.Na haohao hulaumu serikali kwanini wanawachia watu mpaka wanapatwa na maafa.

Kwahiyo ni ngumu sana mtu kuelewa hasa kama utakuwa unasikiliza upande mmoja.Miaka ya nyuma muheshimiwa Makamba aliwahi kuwaambia wakazi wa mabondeni wahame na aliwahi kujitolea mwenyewe kwenda mabondeni kusaidia kubomoa na matokeo yake wanasiasa walikuja juu ili wananchi wafahamu ndio watetezi wao na sio kweli.Mimi siwaamini wanasiasa yeyote yule awe wa chama teule au wapinzani.

Mimi nadhani hawa serikali waamue tu kwamba hakuna ruhusa mtu kurudi huko na waweke ulinzi mkali.Na kinachofuata ni kuzibomoa hizo nyumba na kuwapatia viwanja sehemu salama.Japo tunajua watu hawa wanang'ang'ania kukaa mijini lakini wasiwape nafasi ya kurudi.Na hao wanasiasa wengine waache waseme wee lakini hali ya usalama iwepo kwa hawa viumbe.Nadhani wameanza kubomoa sehemu za Magomeni kama sikosei na itakuwa vizuri kama watatimiza kote kulikojengwa kinyume na sheria.Lakini hali hiyo iwe kwa wote sio kwa walal hoi tu maana kuna wengine wamejenga sehemu za wazi ambazo pia haziruhusiwi kujengwa.