Klabu ya Liverpool imeshauriwa isikate rufaa dhidi ya adhabu ya kufungiwa mechi nane mshambuliaji wao nyota Luis Suarez ambaye amepatikana na hatia ya kutumia maneno ya kibaguzi dhidi ya Patrice Evra wa Man united mwishoni mwa mwaka jana. Piara Powar kutoka Football Against Racism in Europe, alisema kesi hiyo iliyojengeka zaidi katika neno Negrito alilotumia Suarez zaidi ya mara saba katika kipindi kisichozidi mara tatu dhidi ya Patrice Evra, ambapo Suarez amedai kwao South America neno hilo halimaanishi ubaguzi.
Lakini Piara Powar kutuhumiwa kuwa mbaguzi amesisitiza hata kama South America halimaanishi ubaguzi lakini Europe linaleta maana mbaya na ndipo Suarez anapoishi hivyo anapaswa aishi kama wenyeji wake wanavyoishi. Suarez mwenyewe amekaririwa mara kadhaa akidai kuwa amesikitishwa na hasa akidai kuwa yeye ameshakuwa nahodha wa AJAX AMSTERDAM timu amabyo imeundwa na wachezaji wengi weusi pia babu yake yeye Suarez ni mweusi hivyo hawezi kuwa mbaguzi. Lakini mimi binafsi naona Suarez hana utetezi wa maana, kwani unaweza ukawa mbaguzi na bado ukawa na marafiki weusi pia. Na suala si Surez kuwa mbaguzi ila suala ni Suarez kutumia maneno ya kibaguzi dhidi ya Patrice Evra kitu ambacho hakikubaliki.
Piara Powar ameishauri Liverpool isikatae rufaa ambayo kwanza ina nafasi finyu kushinda hivyo itasababisha hasara mbili (1) Suarez kuongezwa mechi za kufungiwa na faini (2) Klabu kubwa kidunia kama Liverpool itapoteza heshima yake kwa kuonekana inamsapoti mchezaji wao ambaye amepatikana na hatia ya kumtusi kirangi mchezaji mweusi. Kama Liverpool haitakuwa makini hili la pili litawagharimu sana kwani ina washabiki wa kila rangi wakiwemo weusi toka duniani kote je? itakuwa inatoa ishara gani kwa mashabiki wao hao?
0 comments :
Post a Comment