News
Loading...

Kwa nini mahala hapa hapana kituo cha dala dala?


Hiki ni kituo cha ubalozi katika barabara ya Ally Hassan Mwinyi
Nimekuwa nikijiuliza kila siku, kwa nini wahusika hawakuweka kituo upande wa kuelekea Selander Bridge katika eneo hili ambapo ukitoka kituo cha Mbuyuni kinachofuata ni Darajani yaani selander bridge, sasa kwa mfano unatokea Morocco na unaelekea ubalozi wa Ufaransa utapaswa ama ushuke Mbuyuni utembee kwa miguu mpaka French Embasy au ukashukie darajani, kwa kutokea Mbuyuni ambapo pana umbali kama wa nusu kilometa ambazo ni nyingi mno kwa kutembea kwa miguu kwa maeneo hayo.  Labda niwaombe tu wahusika waliangalie eneo hilo ambapo nafasi ni nyingi tu za kujenga kituo rasmi kama ilivyo kituo hicho juu pichani. Kutokea DSTV mpaka ulipo ubalozi wa zamani wa Marekani pana nafasi zuinazoweza kutumika. Na wakishafanya hivyo kile cha darajani kiondoshwe tu kwani kitakuwa hakina kazi pale. Tatizo kama hilo pia lipo Kinondoni Rd karibu na STANBIC BANK hapana kituo rasmi japokuwa daladala husimama hapo pande zote za barabara katika vituo visivyo rasmi.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :